Swali: "Je, ninawezaje kuenenda sawa na Mungu?"
Jibu: Ili kuweza kwenenda sawa na Mungu, ni sharti mwanzo tuelewe “makosa” yako wapi. Jibu ni dhambi. “Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la! hata mmoja” (Zaburi 14:3). Tumeasi kwa kukeuka amri za Mungu; Tumekuwa “kama kondoo tumepotea” (Isaya 53:6).
Habari mbaya ni kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. “Roho ile itendayo dhambi itakufa” (Ezekieli 18:4). Habari njema ni kuwa Mungu mwenye upendo alitutafuta ili akatuletee wokovu. Yesu aliapa ya kwamba madhumuni yake ilikuwa ni “kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10), na akatamka madhumuni yake yakuwa imekamilika, wakati alipokufa msalabani, kwa maneno “imekwisha” (Yohana 19:30).
Kuwa na uhusiano wa sawa na Mungu yaanza kwa kutambua dhambi yako. Halafu ifwatilie hali ya kukiri dhambi hiyo mbele za Mungu kwa kunyenyekea (Isaya 57:15) na ujasiri wa kuiacha dhambi hiyo. “Kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10).
Toba hii ni sharti iambatane na imani. Kwa hali ya kipekee, imani yakuwa kifo cha Yesu cha kujitoa na ufufuo wa kiajabu inamwidhinisha kuwa mwokozi wako. “Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Vifungu (vitabu) vyengine vinazungumzia umuhimu wa imani, kama vile Yohana 20:27; Matendo 16:31; Wagalatia 2:16; 3:11, 26; na Waefeso 2:8.
Kuenenda sawa na Mungu ni jinsi utakavyo itikia kwa kile ambacho Mungu ametenda kwa niaba yako. Alituma mkombozi, Alitoa dhabihu ya ondoleo la dhambi yako (Yohana 1:29), na anakupea ahadi: “Na itakuwa kila atakaye liita jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21).
Maelezo mazuri kuhusu Toba na Msamaha ni lile fumbo la mwana mpotevu (Luka 15:11-32). Mvulana huyo mdogo alitapanya urithi aliopewa na babake kwa njia ya uasherati (aya13). Alipotambua makosa yake, aliamua kurudi nyumbani (aya18). Alidhani hangeliweza kuhesabika tena kama mwana (aya19), lakini haikuwa kweli. Babake alipendezwa na kurudi kwake mtoto huyo mwasi, zaidi kuliko mwanzo (aya20), kila kitu alisamehewa na sherehe zikafuatilia (aya24).
Mungu ni mwema kwa kutimiza ahadi zake, hata kwa ahadi ya kusamehe. “Bwana yu karibu na waliopondeka roho huwaokoa” (Zaburi 34:18).
Kama unataka kuenenda sawa na Mungu, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka yakwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile, haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”
Swali: "Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?"
Jibu: Je, unajua kwakweli kua unauzima wa milele na utaenda Mbinguni wakati ukifa? Mungu anataka uwe na uhakika! Bibilia inasema: “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la mwana wa Mungu” (1Yohana 5:13). Kama ungelikuwa umesimama mbele za Mungu saa hii na akuulize, “Kwanini nikuruhusu uingie Mbinguni?” Je, ungelisema nini? Unaweza usijue utajibu nini. Unachohitaji kujua nikwamba Mungu anatupenda na amepeana njia ambapo tunaweza kujua kwakweli ni wapi tutaishi milele.Bibilia inasema hivi “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).
Mwanzo kabisa ni sharti tuelewe shida ambayo inatupinga kufika Mbinguni. Shida ni hii- dhambi yetu ya asili inatupinga kuwa na uhusiano na Mungu. Sisi ni wenye dhambi kiasili na kwa chaguo. “Kwasababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Hatuwezi kujiokoa sisi wenyewe. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu. Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9). Tunastahili mauti na jehanamu. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23).
Mungu ni mtakatifu na mwenye haki na nisharti aadhibu dhambi,kisha anatupenda na amepeana msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi’’ (Yohana 14:6). Yesu alitufia pale msalabani “Kwa maana Kristo naye alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,ili atulete kwa Mungu’’ (1Petro 3:18). Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu nakufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki” (Warumi 4:25).
Sasa turudi kwa swali la kwanza – “Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?’’ Jawabu ni - Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka (Matendo 16:31). Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Unaweza kupokea uzima wa milele kama karama ya bure. “Karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Unaweza kuishi maisha yenye ukamilifu na yenye maana sasa hivi. Yesu alisema mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Unaweza kuishi maisha ya milele na Yesu Mbinguni. “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,nanyi mwep” (Yohana 14:3).
Ukiwa unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na upokee msamaha wa dhambi toka kwa Mungu, hapa kunalo ombi unaweza kuomba. Kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Nikwakumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutakuwezesha kupokea msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kupeana kwa ajili ya msamaha wako.
“Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu ile niliyostahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha! Amina!"
Swali: "Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya Mbinguni?"
Jibu: Mimi ni mtu mzuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni. “Sawa, kwahivyo nafanya mambo mabaya, lakini zaidi nafanya mambo mazuri, kwahivyo nitaenda Mbinguni.” Mungu hatanipeleka Jehanamu kwasababu siishi kulingana na Bibilia. Nyakati zimebadilika!’’ “Watu wabaya pekee kama vile watesaji watoto na wauaji huenda Jehanamu.”
Haya yote ni mafikira ya kawaida kati ya wengi, lakini ukweli ni kwamba yote ni uongo. Shetani mtawala wa dunia, huyapanda mafikira/mawazo haya akilini mwetu. Yeye na yeyote afuataye njia zake ni adui wa Mungu (1Petro 5:8). Shetani hujigeuza na kujifanya mzuri (2Wakorintho 11:14), lakini anauwezo juu ya akili zote ambazo hazimwelekei Mungu. “Shetani, Mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake. Hawaielewi injili kuhusu utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu” (2Wakorintho 4:4).
Ni uongo kuamini ya kwamba Mungu hashuhuliki na dhambi ndogo, na kwahivyo Jehanamu imetengewa “Watu wabaya.” Dhambi zote zinatutenganisha na Mungu, hata “ile dhambi ndogo nyeupe.” Wote wamefanya dhambi, na hakuna atoshaye kuwa mzuri wa kujifikisha Mbinguni yeye mwenyewe (Warumi 3:23). Kuingia Mbinguni haitegemei kwamba uzuri wetu uwe unazidi ubaya wetu, Sote tungelishindwa kama hiyo ndiyo hali. Na ikiwa wanaokolewa kwa neema yake Mungu, basi sio kwa matendo yao mazuri. Kwasababu hiyo, neema yake Mungu isingekuwa kama jinsi ilivyo-ya huru na isiyostahili (Warumi 11:6). Hatuwezi kufanya lolote jema lakutuwezesha kufika Mbiguni (Tito 3:5). Unaweza kuingia katika ufalme wa Mungu kwakupitia mlango ulio mwembamba pekee. Njia ya Jehanamu ni pana na mlango wake ni mpana kwa walio wengi wachaguao njia ya rahisi (Mathayo 3:13). Hata kama kila mtu anaishi maisha ya dhambi, na kumwamini Mungu hakumo, Mungu hatasema hivyo. “Ulikuwa ukiishi kama kawaida ya ulimwengu huu, uliojaa dhambi, ukimtii Shetani mfalme wa uwezo wa anga. Yeye ni roho atendaye kazi katika mioyo ya wale wakataao kumtii Mungu” (Waefeso 2:2).
Wakati Mungu alipoumba ulimwengu, ulikuwa kamili. Kila kitu kilikuwa kizuri. Halafu akamuumba Adamu na Hawa na akawapa uhuru ili waweze kuwa na chaguo kama watamfuata na kumtii Mungu au la. Lakini Adamu na Hawa, wanadamu wa kwanza kabisa Mungu alioumba walidanganywa na Shetani wamuasi Mungu, na wakatenda dhambi. Hii iliwatenganisha (na kila aliyekuja baada yao pamoja na sisi) na uwezo wakuwa na uhusiano wakaribu na Mungu. Yeye ni mkamilifu na hawezi kuwa penye dhambi. Kama watu wenye dhambi, hatungeliweza kufika huko sisi wenyewe kwahivyo, Mungu akatengeza njia ili tuweze kupatanishwa naye huko mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Yesu alizaliwa ili aweze kutufundisha / kutuonyesha njia na afe kwa ajili ya dhambi zetu. Siku tatu baada ya kifo chake, alifufuka toka kaburini (Warumi 4:25), akishuhudia ushindi wake juu ya mauti. Aliliunganisha pengo kati ya Mungu na mwanadamu ili tukaweze kuwa na uhusiano wa kibinafsi naye kama tutaamini.
“Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana17:3). Watu wengi wamwamini Mungu, hata Shetani pia. Lakini kupokea wokovu, ni sharti tumregelee Mungu, tujenge uhusiano wa kibinafsi, tuziache dhambi zetu na tumfuate yeye. Ni sharti tumwamini Yesu kwa kila kitu tulicho nacho na kwakila tunachofanya. “Tunafanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu tunapomwamini Yesu Kristo atuchukulie dhambi zetu. Na sote tunaweza kuokolewa namna hii, haijalishi sisi ni kina nani au tumefanya nini’” (Warumi3:22). Bibilia inafundisha yakuwa hakuna njia nyengine yoyote ya wokovu isipokuwa kupitia kwa Kristo. Yesu asema katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Yesu ndiye njia ya pekee ya wokovu kwasababu yeye pekee anaweza kutulipia adhabu ya dhambi zetu (Warumi 6:23). Hakuna dini nyengine yoyote ifundishayo kwa kina au uzito wa dhambi na madhara yake. Hakuna dini nyengine yoyote inayogarimia malipo ya dhambi isipokuwa Yesu pekee. Hakuna “mwanzilishi wa dini” mwengine ambapo Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana1:1, 14) - njia ya pekee ya kuweza kulipa deni. Ilibidi Yesu kuwa Mungu ili aweze kutulipia deni. Ilibidi Yesu afanyike kuwa mwanadamu ili aweze kufa. Wokuvu unapatikana kwa imani ndani ya Yesu Kristo! “Wala hakuna wokovu katika mwengine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya Mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).
05/02/15
Swali: "Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?"
Jibu: Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”
Msamaha ni nini na kwanini ninauhitaji?
Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia, kufutilia mbali deni. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili tukarudishe uhusiano. Msamaha haupeanwi kwa sababu mtu anastahili kusamehewa. Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha ni ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi wa kutoshikilia jambo ndani yako kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.
Bibilia inatuambia yakwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20 asema, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8 asema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46;Yohana 3:36).
Msamaha-Je, ni upate vipi?
Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye ari ya kutusamehe dhambi zetu! 2Petro 3:9 asema, “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alitoa kwa ajili ya msamaha wetu.
Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Warumi 6:23 yasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo ndiyo tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe? Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu ku epukika?Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako. Waefeso1:7 yasema, “katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe! Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajab, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Msamaha-Je, ni jambo lililo rahisi?
Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weak imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu/ya ajabu na kwa msamaha! Amina.”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
Je, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?
Swali: "Je, ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo?"
Jibu: Je ina maanisha nini kuzaliwa mara ya pili kwa mkristo? Sehemu muhimu katika Bibilia inyo jibu swali hili ni Yohana 3:1-21. Bwana Yesu Kristo akizungumza na Nikodemo mkuu kati ya mafarisayo na mfuasi katika kikao (mahakama) kikuu cha wayahudi (Mfalme wa wayahudi). Nikodemo alikuwa amemjia Yesu usiku. Nikodemo alikuwa na maswali ya kumuuliza Yesu.
Wakati Yesu akizungumza na Nikodemo, alisema, Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?” “Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin, Amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili…” (Yohana 3:3-7).
Msemo “kuzaliwa mara ya pili” unamaanisha “zaliwa toka juu” Nikodemo alikuwa na uhitaji wa kweli. Alihitaji mabadiliko ya moyo wake... Mabadiliko ya kirohoUzao mpya, kuzaliwa mara ya pili, ni kitendo au hatua ya Kiungu ambapo uzima wa milele hupewa mtu yule aaminiye (2Wakorintho 5:17; Tito 3:5; 1Petro 1:3; 1Yohana 2:29; 3:9; 4:7; 5:1-4, 18). Yohana1:12, 13 inasema ya kuwa”kuzaliwa mara ya pili” pia ina maana “kufanyika mtoto wa Mungu”kwa imani katika jina la Yesu Kristo.
Swali hasa ni kuwa, “kwa nini mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili?” Mtume Paulo katika Waefeso 2:1 asema, “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi …” Kwa Warumi katika Warumi3:23, Mtume aliandika, ”kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. “Kwahivyo mtu anahitaji kuzaliwa mara ya pili ili asamehewe dhambi zake na awe na uhusiano na Mungu.
Je, hii hutokea vipi? Waefeso2:8, 9 yasema, kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu.” Mtu anapo “okolewa”, basi yeye amezaliwa mara ya pili, akijazwa upya kiroho, na sasa amefanyika kuwa mwana wa Mungu kwa haki ya uzao mpya. Kwa kumwamini Kristo Yesu, yeye aliye adhibiwa kwa ajili ya dhambi alipokufa msalabani, ndiyo maana ya “kuzaliwa mara ya pili” kiroho. “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya…” (2Wakorintho 5:17 a).
Kama bado hujaweza kumwamini Bwana Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako, je utakuwa na utayari wa kupokea Roho mtakatifu wakati akizungumza na moyo wako? Unahitaji kuzaliwa mara ya pili. Je, utaomba maombi ya kutubu na ufanyike kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo hivi leo? “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12-13).
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako na uzaliwe mara ya pili, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-karama ya uzima wa milele! Amina!”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?
Swali: "Je, ni gani sheria hizi Nne za Kiroho?"
Jibu: Sheria hizi Nne za kiroho ni njia za kushiriki habari njema za wokovu upatikanao kupitia imani ndani ya Yesu Kristo. Ni njia moja rahisi ya kupanga habari muhimu katika injili kwa sehemu Nne.
Ya kwanza kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Mungu anakupenda na ana mpango wa ajabu juu ya maisha yako.” Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 10:10 yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Ni kitu gani kinachotuzuia na upendo wa Mungu? Ni kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?
Ya pili kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Hali ya Utu wa mwanadamu inachafuliwa na dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa matokeo haya basi, hatuwezi kamwe kuufahamu mpango wa ajabu alio nao Mungu juu ya maisha yetu.” Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 6:23 inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.” Mungu alituumba ili tukaweze kuwa na ushirika naye. Hata hivyo hali ya Utu/Ubinadamu ilileta dhambi katika dunia, na hivyo basi kutengwa na Mungu. Tumeharibu uhusiano pamoja naye ambao Mungu alikusudia tukaupate. Je, suluhisho ni nini?
Ya tatu kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Yesu Kristo ndiye toleo la Mungu pekee kwa ondoleo la dhambi zetu. Kupitia kwa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika wa haki na Mungu.” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko….” Yesu mwenyewe akiri yakwamba yeye ndiye njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Je, ninawezaje kupata kipawa hiki kikuu cha wokovu?
Ya Nne kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Ni sharti tuweke imani yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea kipawa cha wokovu na kujua mpango wa ajabu wa Mungu juu ya maisha yetu. Yohana 1:12 inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. “Matendo16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka!” Tunaweza kuokolewa kwa neema peke yake, kwa njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya haitakuokoa, lakini itawezekana kwa kumwamini Kristo!Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kum shukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
Swali: "Je umepata uzima wa milele?"
Jibu: Bibilia inaonyesha njia ya wazi ya uzimani.Mwanzo ni sharti tutambue yakwamba tumetenda dhambi kinyume chake Mungu: “Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Sote tumefanya mambo ambayo hayampendezi Mungu,ambayo yanafanya tustahili adhabu.Kwa kuwa dhambi zetu ziko kinyume kabisa na Mungu aliye uzima wa milele,basi ni adhabu ya milele pekee itoshayo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Hata hivyo Yesu Kristo asiyekuwa na dhambi (1 Petro 2:23), mwana wa Mungu alifanyika kuwa mwanadamu (Yohana 1:1,14) na akafa ili kutulipia adhabu. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi,kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8). Yesu Kristo alikufa msalabani (Yohana 19:31-42), kwa kuchukua adhabu ambayo sisi tulistahili (2Wakorintho 5:21). Siku tatu baadaye akafufuka katika wafu (1Wakorintho 15:1-4), kudhihirisha ushindi juu ya dhambi na mauti. “kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu” (1Petro 1:3).
Kwa imani ni sharti tuungame dhambi zetu na tumrejee Kristo kwa ajili ya wokovu (Matendo 3:19). Tukiweka imani yetu kwake, kwa kuamini kifo chake msalabani kama malipo ya dhambi zetu,tutasamehewa na kuahidiwa uzima wa milele mbinguni. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa sababu,ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Imani pekee katika kazi aliyo ikamilisha Kristo pale msalabani ndiyo njia ya kweli ya pekee ya uzimani! “Kwa maana nimeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yoyote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumpokea Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako,tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haitakuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo peke yake ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumuelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu,najua yakwamba nimetenda dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Nina ziacha dhambi zangu na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu /ya ajabu na kwa msamaha - karama ya uzima wa milele! Amina!”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
|
|